AINA ZA MANENO
Katika lugha ya Kiswahili kuna angalau aina nane za maneno ambazo wataalamu wengi wa lugha wanakubaliana hivyo. Katika mada hii utaweza kujifunza na kubainisha aina zote nane za maneno na jinsi zinvyotumika katika sentensi. Utaweza pia kujifunza namna ya kutofautisha aina za maneno ambazo zimeleta ubishi miongoni mwa wataalamu wengi hususani katika Viunganishi na Vihusishi.
Aina
Saba za Maneno ya Kiswahili
Aina za maneno katika lugha ya Kiswahili ni pamoja na hizi zifuatazo:
Aina Nomino (N)
Viwakilishi (W)
Vitenzi (T)
Vivumishi (V)
Vielezi (E)
Viunganishi (U)
Vihusishi (H)
Vihisishi (I)
Ufafanuzi wa Aina za Maneno
1. NOMINO (N)
Nomino ni maneno yanayotaja vitu, watu, na hali kadhalika. Kuna aina mbali mbali za maneno ambazo ni pamoja na hizi zifuatazo:
1. Nomino za pekee
Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino mahsusi na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si kingine chochote. Hizi ni nomino zinazohusisha majina kama vile ya watu, nchi, miji, mito, milima, maziwa na bahari. Herufi za kwanza za nomino za pekee huwa kubwa hata kama nomino hizi zinapatikana katikati ya sentensi.
2. Nomino za kawaida
Hizi kwa jina jingine huitwa nomino za jumla. Nomino hizi hazibainishi wazi wazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa mfano ikiwa ni mtu, mahsusi hatambuliwi. Haituambii kama ni Bahati, Bite ama Neema. Ikiwa ni mlima hautambuliwi kama ni Meru , Kilimanjaro au Evarest, yaani hutaja vitu bila kutaja umahususi wake kama ilivyo katika nomino za pekee.Hizi zinapoandikwa si lazima zianze na kwa herufi kubwa ispokuwa zimetumiwa mwanzoni mwa sentensi au zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vile Mkuu wa Sheria. Katika mfano huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida, lakini hapa inaanza kwa herufi kubwa kwani inataja anuwani ya kipekee.
3. Nomino za mguso
Nomino za mguso hurejelea vitu vinavyoweza kuhusika na mwanadamu kupitia milango ya hisia kama macho, mapua, masikio vidole na ulimi- yaani vitu vinavyoweza kushikika, kuonekana, kunusika na kuonjeka.
4. Nomino za jamii
Hizi ni nomino ambazo zinawakilisha vitu vingi katika jina moja, yaani nimino zinazotaja umla ya vitu vingi. Mfano; jozi ya viatu, umati wa watu, bustani ya maua, bunga ya wanyama
5. Nomiono dhahania:
Kundi hili la nomino hutumia kigezo cha uwezekano wa kuhesabika kuziainisha. Hapa tunatofautisha kati ya nomino zinazowakilisha vitu vinavyohesabika kwa upande mmoja, na vile visivyohesabika kwa upande mwengine. Nomino ya vitu vinavyohesabikavitanda, nyumba,vikombe vitabu na kadhalika.Zile zisizohesabika hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haviwezi kugawika, kwa mfano maji, mate, makamasi, maziwa, moshi, mafuta. Aghalabu nomino hizo huwa sawa katika umoja na wingi.
6. Nomino za kitenzi jina:
Hizi ni nomino zinazohusu vitenzi. Huundwa kwa kuongezwa kiambishi {ku-} cha unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe nomino.
2. VIVUMISHI (V)
Vivumishi ni maneno yanayoelezea zaidi juu ya nomino, aghalabu vivumishi hutanguliwa na nomino. Kuna aina kadhaa za vivumushi, miongoni mwa hivyo ni pamoja na hivi vifuatavyo.
Vivumishi vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo
1. Vivumishi vya sifa. Hutoa sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi huweza kuwa nzuri, mbaya au yoyote ile.
2. Vivumishi vya idadi. Vivumishi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino. Kuna vivumishi vya idadi vinavyoweza kuvumisha nomino kwa kutaja idadi ya nomino hizo kiujumla jumla bila kudhihirisha idadi halisi.
3. Vivumishi vya idadi ambavyo huonyesha nafasi iliyochukuliwa na nomino fulani katika orodha.
4. Vivumishi vya kumiliki: Ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina milikiwa na mtu au kitu kingine.
5. Vivumishi Vioneshi. Vivumishi vya aina hii huonyesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi vya aina hii hujengwa na mzizi{h}kwa vitu vilivyopo karibu na mzizi{le}kwa vitu vilivyo mbali.
6. Vivumishi vya kuuliza: Hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari zake. Hujibu swali “gani? ipi? ngapi?”
7. Vivumishi vya A- unganifu: Vivumishi vya aina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a- unganifu. Kihusishi hiki huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho huvumisha nomino iliyotajwa awali.Vivumishivya aina hii hutumika kuleta dhana za–Umilikaji, - Nafasi katika orodha.
8. Vivumishi vya jina kwa jina: Hizi ni nomino zinazotumika kama vivumishi ambazo hutumika kufafanua nomino
9. Vivumishi vya pekee. Vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojawapo huwa na maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli ya nomino ambayo kinaivumisha.
Mizizi vivumishi hivi niote, o-ote, -enye, -enyewe, -ingine, -ingineo.
- ote:Huonyesha ujumla wa kitu au vitu
- o-ote:Kivumishi cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila kubagua”
– enye:Kivumishi cha aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino fulani.
- enyewe:Kivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani.
– ingine:Kivumishi cha aina hii huonyesha/huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu fulani
– ingineo:Kivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonyesha ziadi.
3. VIELEZI (E)
Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi au vielezi vingine. Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi, namna gani na hata mara ngapi.
Aina za vielezi
1. Vielezi vya Mahali. Vielezi vya mahali hutoa habari kuhusu mahali ambapo kitendo kilifanyika. Aghalabu vielezi hivi huundwa kwa kutumia jina la mahali au kwa kuongeza kiungo -NI mwishoni mwa neno linaloashiria mahali.Kwa mfano:nyumbani, kazini, shuleni
Example
1. Mtoto huyo hajatulia nyumbani tangu alipotoka Mombasa.
2. Msipitie sokoni mkienda kanisani.
2. Vielezi vya Wakati. Huelezea zaidi kuhusu wakati kitendo kinapofanyika; kwa mfano: jioni, jana, asubuhi, saa saba, mwaka juzi.
Example
1. Mzee Kasorogani amesema kwamba ataoga mwaka ujao
2. Musa alilazimishwa kuchimba mtaro saa sita usiku
3. Kisaka na Musa watakutana kesho
3. Vielezi vya Idadi. Vielezi vya idadi hutulezea kitendo kilifanyika mara ngapi.
a) Idadi Kamili: Vielezi vya Idadi Kamili hutaja idadi kamili ya mara ngapi kitendo kilifanyika. Kwa mfano:mara mbili, siku mbili kwa juma, mara kumi
Example 1
1. Gibi alimzaba kofi mara tatu na kisha akakimbia
2. Daktari alimwagiza mama huyo achukue dawa mara tatu kwa siku na arudi hospitalini siku mbili kwa mwezi
b) Idadi Isiyodhihirika: Vielezi vya Idadi Isiyodhirika huelezea kiasi ambacho kitendo kilifanyika bila kutaja kiasi kamili kwa mfano:chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani.
Example 2
Mwizi wa kuku alipigwa mara kadhaa kabla ya kuokolewa na polisi.
Yeye hunipigia simu mara kwa mara.
4. Vielezi vya Namna au Jinsi. Vielezivya namna hii huonyesha jinsi au namna kitendo kilivyotendeka. Vielezi vya namna vipo vya aina kadhaa.
5. Vielezi vya Namna Halisi. Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa moja katika uainishaji wa aina za maneno.
6. Vielezi vya Namna Mfanano. Hivi ni vieleziambavyo hutumika kufananisha vitendo na vivumishi au nomino mbalimbali. Hujengwa kwa kuongeza kiambishi(ki-) au kiambishi(vi-).Viambishi hivi hujulikana kwa jina la viambishi vya mfanano.
Mfano; Ulifanyavizurikumsaidia mwanangu.
7. Vielezi vya Namna Vikariri. Hivi ni vielezi ambavyo hufafanua vitenzi kwa kurudiarudia neno moja mara mbili.
8. Vielezi vya Namna Hali. Hivi ni vielezi ambavyo hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka kimetendeka katika hali gani.
9. Vielezi vya Namna ala/kitumizi. Hivi ni vielezi vinavyotaja vitu ambavyo hutumika kutendea kitendo
10. Vielezi vya Namna Viigizi. Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha sauti inayojitokeza wakati tendo linapofanyika au kutokea.
11. Vielezi vya Wakati. Vielezivya namna hii huonyesha wakati wa kutendeka kwa kitendo.Huweza kutokea kama maneno kamili au hodokezwa kwa kiambishi{po}
4. VITENZI
Kitenzi ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti
Aina za Vitenzi
1. Vitenzi vikuu: Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbe muhimu wa kiarifu cha sentensi.
2. Vitenzi visaidizi: Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile uwezekano , wakati, hali n.k.Vitenzi visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba viambishi vya wakati.
3. Vitenzi vishirikishi: Hivi ni vitenzi vishirikishi ambavyo havichukui viambishi vya nafsi, njeo ama hali. Vitenzi vishirikishi vipungufu ni vya aina mbili, ambavyo ni kitenzi kishirikishi“ni” cha uyakinishina kitenzi shirikishi “si” si cha ukanushi.
4. Vitenzi vishirikishi vikamilifu: Hivi huchukuwa viambishi viwakilishi vya nafsi, njeo na hata hali. Kwa mfano;ndiye, ndio, ndipo.
Kazi za Kitenzi Kikuu
1. Kueleza tendo linalofanywa na mtenda/mtendwa.
2. Kuonyesha wakati tendo linapotendeka
3. Kuonyesha hali ya tendo
4. Kuonyesha nafsi
5. Kuonyesha kauli mbali mbali za tendo
6. Kuonyesha urejeshi wa mtenda/mtendwa/ mtendewa/ kujitendea
Kazi za Kitenzi Kishirikishi
1. Kushirikisha vipashio vingine katika sentensi
2. Kuonyesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu fullani.
3. Kuonyesha cheo au kazi anayofanya mtu.
4. Kuonyesha sifa za mtu.
5. Kuonyesha umoja wa vitu au watu
6. Kuonyesha mahali
7. Kuonyesha msisitizo
8. Kuonyesha umilikishi wa kitu chochote.
Aina za Wakati Katika Kitenzi
- Wakati uliopita
- Wakati uliopo
- Wakati ujao
Hali mbalimbali za kitenzi
- Hali ya masharti
- Hali ya kuendelea kwa tendo
- Hali ya kutarajia, kuamuru na kuhimiza
5. VIWAKILISHI
Viwakilishi ni aina ya neno linaloweza kutumika badala ya jina/nomino .
Aina za Viwakilishi
1. Viwakilishi vioneshi au viwakilishi vya kuonesha. Viwakilishi vionyeshi hutumika badala ya nomino kwa kutumia kuonyesha nomino inayorejelewa bila kuitaja. Kwa mfano; huyu, yule, hapo, kule, humo. Huyu si mwenzetu kabisa; kule hakufai kwenda watoto.
2. Viwakilishi vya nafsi: Kwa mfano: mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi, wao
3. Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viulizi. Ambavyo huashiriwa na mofu /kiambishi{-pi}ambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina husika. Kwa mfano, Wangapi wameondoka? Kipi kimekosewa?
4. Viwakilishi vya urejeshi. Ambavyo vinajengwa na shinaambapamoja na vipande vidogo vidogo –ye-, -o-, -cho-, vyo, lo, po, mo, kon.k ambavyo vinachaguliwa kulingana na ngeli ya majina yanayorejeshwa navyo. Mfano; aliyeondoko hatapewa chake.
5. Viwakilishi vya idadi: Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino hiyo huweza kuwa kamili (halisi) au ya jumla.
6. Viwakilishi vya pekee/vimilikishi. Hivi ni aina ya vivumishi vya pekee kuwakilisha nomino. Hufuata sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa. Mfano; '-angu, -ako, -ake, -etu, -enu, -ao '. kwangu haingii megini, chako haikna thamani.
7. Viwakilishi vya A-Unganifu. Viwakilishi hivi huundwa kwa kihusishi chaA-unganifukusimamia nomino iliyomilkiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au nomino ya aina fulani. Kihusishi a-unganifu huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho husimama mahali pa nomino. Mfano;ya kwakeyamemshinda,vya wazeehaviguswi.
8. Viwakilishi vya sifa: Haya ni maneno ya sifa ambayo huchukua nafasi ya nomino katika setensi. Kwa mfano -eupe, -janja, -tamu
7. Viwakilishi vya Idadi. Idadi Kamili- hutumia namba kuelezea idadi ya nomino. 'saba, mmoja, ishirini' -Hutumika kusimama badala ya nomino kwa kurejelea idadi yake. Idadi Isiyodhihirika- huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja idadi kamili: 'chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani'
6. VIUNGANISHI
Ni maneno, kikundi cha maneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi au sentensi.Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi.
Aina za Viunganishi
1. Viunganishi huru: hivi ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo, katikati ya vipashio vinavyoungwa.Viunganishi huru hujumuisha:
2. Viunganishi nyongeza/vya kuongeza, kama vile, na, pia, pamoja. Baba na mwanae wanacheza mpira, Alichukua chakula chote pamoja na akiba iliyokuwepo.
3. Viunganishi vya sababu/visababishi, mfano, kwa sababu, kwa kuwa, kwa vile, madhali, ili. Alimsogelea karibu ila ambusu, Atatumikia kifungo madhali amebainika kuwa na hatia.
4. Viunganishi vya uteuzi/chaguo. Mfano; au, Naweza kwenda nyumani au shuleni.
5. Viunganishi vya kutofautisha/vya kinyume:ila, lakini, kinyume na, japokuwa, ingawa, ilihali. Mfano; Mkumbatie lakini usimbusu.
6. Viunganishi vya wakati. Wakati mfano; Mwalimu aliuliza swali wakati yeye amesinzia.
7. Viunganishi vya masharti; ikiwa, iwapo, hadi. Mfano; utaruhusiwa kuingia hapa ikiwa umevaa mavazi yanaostahili.
8. Viunganishi vihusishi; miongoni mwa, kati ya; mfano: Jane alikuwa miongoni mwa washindi kumbi bora kitaifa.
9. Viunganishi tegemezi: ni viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano au shurtia. Mfano; -po-, -cho-, -o- Nili-po-amka…, Ali-cho-mwelez…, alizo-o-neshwa…n.k
7. VIHUSISHI
Ni maneno ambayo huonyesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na jingine. Vihusishi aghlabu huonyesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino na maneno mengine.
Mambo yanayoweza Kuonyeshwa na Vihusishi
1. Huonyesha
uhusiano wa kiwakati; Mfano, ni vizuri kupiga mswakibaada yachakula.
2. Huonyesha uhusiano wa mahali: mfano, Ninaishikaribu nakwa Mtogole
3.
Huonyesha uhusiano wa kulinganisha: Amekulazaidi yauwezo wake.
4. Huonyesha uhusiano wa umilikaji: Usiguse hicho kitabu nicha kwangu
5. Huonyesha uhusiano wa sababu/kiini: nimerudi kwaajili yakuonana na mkuu wa shule.
Aina za Vihusishi
1. Vihusishi vya wakati
2. Vihusishi vya mahali
3. Vihusishi vya vya kulinganisha
4. Vihusishi vya sababu
5. Vihusishi vya ala/kifaa mfano; kwa
6. Vihusishi vimilikishi
7. vihusishi vya namna; Kichwacha mviringo
8. Vihusishi ‘na’ cha mtenda mfano, amepigwana Juma.
Matumizi ya kihusishi “kwa”
1.
Huonyesha mahali au upande: Mfano, amekwenda kwa mjomba wake.
2. Huonyesha sababu au kisababishi cha jambo: mfano; ninaishi kwa ajili yako.
3. Huonyesha wakati: mfano; sina nafasi kwa sasa.
4. Huonyesha sehemu fulani ya kitu kikubwa, mfano: Mpira umekwisha wakiwa wamefungana nne kwa tatu.
5. Huonyesha jinsi kitendo kilivyotendeka: Mfano; alimvuta kwa nguvu sana ndo maana limevunjika.
8. VIHISISHI/VIINGIZI
Ni maneno ambayo hutumiwa kuwakilisha hisia fulani.
Vihusishi vinaweza kugawanywa katika makundi yafuatayo:
1. Vihisishi vinavyoonyesha mhemko au hisi kali
2. Vihisishi vya furaha
3. Vihisishi vya huzuni
4. Vihisishi vya mshituko
5. Vihisishi vya mshangao
Vihisishi vya maamrisho au msisitizo wa jambo au tukio
1. Vihisishi vya maadili
2. Vihisishi vya mwiitiko
3. Vihisishi vya ombi
4. Vihisishi vya bezo
5. Vihisishi vya kutakia heri
6. Vihisishi vya kukiri afya/jambo
7. Vihisishi vya kiapo
8. Vihisishi vya salamu
Matumizi ya Aina za Maneno katika Tungo
Aina za maneno hutumika katika tungo kwa kutegemeana na lengo la msemaji. Kwa mfano kama lengo la msemaji ni kuonesha aina fulani ya hisia atatumia vihisishi katika tungo yake. Vilevile kama msemaji anahitaji kueleza kuhusu namna nomino inavyotenda, ilivyotendewa au inavyotendwa, atatumia kitenzi.
MATUMIZI YA KAMUSI
Kamusi ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani na kupangwa katika utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo wasomaji wanaweza kuelewa. Au kamusi ni orodha ya maneno yaliyo katika karatasi au nakala tepe yaliyopangwa kialfabeti na kutolewa maana pamoja na maelezo mengine na kuhifadhiwa katika kitabu, santuri, simu, tarakilishi au katika mfumo wowote wa kielekroniki. Kamusi huweza kuwa ya lugha moja, yaani orodha ya maneno pamoja na maelezo yake yakiwa katika lugha moja
Example 1
Mfano: chatu ni nyoka mkubwa na mnene
Kamusi nyingine huwa za lugha mbili yaani orodha ya maneno ipo katika lugha moja na maelezo ya maana ya maneno hayo yapo katika lugha nyingine.
Example 2
chatu, n python
Kamusi ni hazina ya lugha inayohusika, kwani tofauti na vitabu vingine vya lugha, huwa na orodha ya maneno mbali mbali yanayotumiwa na wazungumzaji wa lugha ile pamoja na maana zake. Japokuwa wingi wa maneno hutegemea ukubwa wa kamusi, kitabu hiki kina manufaa makubwa kwa mtumiaji wake kwani humpatia msamiati asioufahamu pamoja na maana zake au humpatia maana zaidi ya maneno anayoyafahamu.
Taarifa zinazopatikana katika Kamusi
Awali kamusi zilipoanza kutungwa zilikuwa ni orodha ya maneno magumu pamoja na maana zake. Kamusi za siku hizi huwa na taarifa zaidi ya maana. Miongoni mwa taarifa ambazo kamusi huwa nazo ni:
1. Tahajia za maneno mfano. Tasinifu Vs Tasnifu, Burangeti Vs Blanketi, Kula Vs Kura, -ingine vs -engine
2. Matamshi
3. Sarufi ya lugha kama inavyojitokeza katika kila neno kama vile maumbo ya wingi wa nomino, vinyambuo vya neno kama vile chezesha, chezeka, chezea, mchezo, mchezajin.k ambavyo vinatokana na kitenzi cheza
4. Maana
5. Etimolojia ya neno (asili ya neno husika)
6. Matumizi ya neno
Jinsi ya Kutumia Kamusi
Maneno yanayoingizwa katika kamusi hupangwa kwa utaratibu wa alfabeti. Maneno yanayoanza na herufi a, yote huwekwa chini ya herufi A. Maneno yanayoanza na herufi fulani nayo hupangwa katika utaratibu wa alfabeti kwa kuzingatia herufi ya pili, ya tatu, nne au tano ya neno kama mfano hapa chini unavyoonyesha.
Example 1
Mfano:ja, jabali, jabiri, jadhibika, jadi.
Maneno yote yanaanza na herufi [j]. herufi ya pili kwa maneno yote ni [a]. herufi ya tatu ni [b] na [d]. Kwa kuwa [b] hutangulia [d] katika mpangilio wa alfabeti maneno yenye [b] kabla ya yale yenye [d]. Kwa kuwa maneno yenye herufi [b] ni mawili itabidi tutazame herufi ya nne ya hya maneno ili tuchague litakaloorodheshwa mwanzo. Neno ‘jabali’ litaorodhewshwa kabla ya ‘jabiri’ kwa kuwa [a] (herufi ya nne) ya ‘jabali’ hutangulia [i] ya ‘jabiri’ ambayo pia ni herufi ya nne. Kisha tunatazama maneno yenye [d] kama herufi ya tatu. Hapa tunaangalia pia herufi ya nne ili kubaini neno litakaloandikwa mwanzo kati ya ‘jadhibika’ na ‘jadi’. Kwa kuwa [h] hutangulia [i] basi ‘jadhibika’ huorodheshwa mwanzo ndipo lifuatiwe na ‘jadi’.
Kwa hiyo hivi ndivyo unavyopaswa kutafuta neno kwenye kamusi. Nenda kwenye herufi ya neno unalotafuta alafu litafute kwa kufuata mlolongo huo huo wa herufi ya kwanza kuorodheshwa.
Neno linaloorodheshwa kwenye kamusi ili lifafanuliwe linaitwakidahizo.Kidahizo huandikiwa maelezo ya kukifafanua. Maelezo haya ni matamshi ya kidahizo, maana ya kidahizo, kategoria ya kisarufi, sentensi ya mfano wa matumizi ya kidahizo n.k. Kidahizo pamoja na maelezo yake ndio huitwakitomeo cha kamusi.
Example 2
Kitomeo cha kamusi
Dhabihu (kidahizo) nm (kategoria ya neno) mahali pa kuchinjia wanyama (maana ya neno).
Taarifa Ziingizwazo katika Kamusi
Fafanua taarifa ziingizwazo katika kamusi
Maana za maneno
Kwa mfano: Dhabihu nm mahali pa kuchinjia wanyama.
Kategoria za Maneno
Kategoria za maneno kama vile kielezi (ele), kitenzi (kt), kivumishi (kv), nomino (nm), kihisishi.
Mifano ya Matumizi
Kwa mfano, Waiziraeli huwapeleka koondo wao kwenye dhabihu kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Lengo la kutoa mifano ni kumsaidia msomaji asiye fahamu vyema neno husika aelewe jinsi neno hilo linavyotumika.
Uingizaji wa nomino
Nomino nyingi katika lugha ya kiswaili zina maumbo ya umoja na wingi.
Mfano: dume nmma-
mkopo; nm mi-
Viambishi ambatishi huwekwa kando ya nomino kuashiria umbo la wingi la nomino.
Ngeli za nomino
Mfano: mkopo nmmi- [u-/i-]
Kutafuta maana unayoitaka
Neno linaweza kuwa na maana moja au zaidi ya moja. Maana inapokuwa moja mtumiaji kamusi hana tatizo kwani hiyo ndiyo atakayoipata na kuichukua. Lakini neno linapokuwa na maana zaidi ya moja, mtumiaji kamusi hutatizika asijue ni ipi aichague. Ili kupata maana inayosadifu itafaa mtumiaji kamusi kutafuta maana ambayo inahusiana na muktadha wa neno linalotafutwa.
Mfano: kifungo nm vi-
1. Kitu cha kufungia
2. Kitu kinachotumiwa kufungia vazi kama vile shati, gauni, suruali n.k
3. Adhabu ya mtu kuwekwa jela kwa muda fulani
Iwapo mtumiaji aliona neno ‘kifungo’ kwa muktadha wa: “Juma alihukumiwa kifungo cha miaka kumi baada ya kupatikana na hatia ya kubaka….” Maana ya mukatadha huu itakuwa ni ile maana ya 3 kwa sababu ndiyo yenye kuhusiana na muktadha ambapo neno kifungo limetumika na wala sio maana ya 1 wala ya 2.