Skip to main content

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA - UFAHAMU

 UFAHAMU



Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma.

 

KUSIKILIZA

 

Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe.

 

Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa Kusikiliza

 

Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:

 

1. Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa

 

2. Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza

 

3. Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa.

 

Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:

 

1. Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila anachokisema.

 

2. Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.

 

3. Msomaji anatakiwa kuandika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya muhimu ili kumasidia kukumbuka hapo baadae.

 

4. Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono, kutingisha kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi huwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.


Zoezi 1

Jibu maswali kutokana na habari uliyosikiliza

 

KUSOMA KWA SAUTI

 

Kusoma kwa sauti ni namna ya kuyaangalia maandishi na kuyatamka kwa sauti inayosikika. Kuna vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:

1. Uelewa wa msamiati na 

2. Uelewa wa matini

 

Ili kuilelewa habari/matini ni lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati uliotumika katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka vilevile matini yote haitaeleweka.

 

Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa Kusoma kwa Sauti

 

Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:

 

1. Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatakiwa ajiulize, Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo.

 

2. Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatazingatia alama za uakifishaji anaweza kupotosha maana ya mwandishi.

 

3. Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia kuelewa vyema maana ya mwandishi.

 

4. Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele anachokisoma inampasa akielewe vizuri.

 

Kwa kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.

 

Zoezi 2

Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma

 

KUSOMA KIMYA

 

Katika usomaji huu, msomaji hufumba kinywa na kupitisha macho katika kila mstari harakaharaka. Macho hayo huunganisha neno lililotangulia na lile linalofuata. Ubongo wake huchambua mambo muimu yanayojitokeza, huku akiyahifadhi kichwani. Mtu akijizoeza kusoma kimya, ananufaika ifuatavyo:

 

1. Hupata nafasi ya kupima mwendo wake na kiasi cha welewa

 

2. Hujiepusha na lawama ya kusumbua wengine

 

3. Hukwepa kuzingatia kanuni za matamshi

 

4. Huweza kusoma maandishi mengi kuliko ambavyo angesoma kwa sauti


KUSOMA KWA BURUDANI

 

Huu ni usomaji ambao lengo lake kuu huwa ni kujiburudisha tu. Katika usomaji wa aina hii, msomaji hujisomea zaidi magazeti, majarida na vitabu tofauti na vile vinavyotumika darasani.

 

Mambo ya Kuzingatiwa katika Ufahamu wa Kusoma kwa Burudani

 

Wakati mwingine sio lazima msomaji awe na vitabu vyote ambavyo anahitaji kuvisoma au magazeti na majarida. Inapotokea hivyo, msomaji anaweza kwenda maktaba kuazima kitabu nachokihitaji.

 

Ingawa lengo la msomaji huwa ni kujiburudisha tu, lakini pia hujiongezea maarifa. Hii ni kwa sababu, magazeti, majarida na vitabu sambamba na kutuamia lugha sanifu huelezea mambo mabalimbali yanayoihusu jamii.

 

Hivyo msomaji kutokana na kusoma vitabu na majarida mbalimbali hujiongezea kiwango cha welewa wa lugha na mambo mengine ya kijamii yanayojadiliwa humo.

 

Ni jambo zuri kwa msomaji kujijengea tabia ya kujipima ili aweze kuelewa kiwango cha maarifa aliyopata katika kujisomea. Kujipima huku kunaweza kufanywa kwa kujiundia utaratibu wa kuweka kumbukumbu ya vitu au makala zilizosomwa na kufanya ufupisho wa kila makala.

 

Utaratibu unaopendekezwa katika kujipima na kujiwekea kumbukumbu ya usomaji wa burudani ni kama ufuatao:

 

1. Tarehe .....

2. Jina la kitabu/makala/gazeti ...

 

3. Mchapishaji ....

4. Mwaka/tarehe ya uchapishaji ....

 

5. Ufupisho wa habari(yasizidi maneno 20) 

6. Fundisho/ujumbe mkuu ni ... 

 

7. Jambo lililokuvutia sana .....

8. Maoni kwa ujumla kama yapo .....

 

 

Popular posts from this blog

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA - UANDISHI WA BARUA

   UANDISHI WA BARUA     Uandishi Wa Barua   Barua za kirafiki ambazo pia huitwa za kidugu huandikwa baina ya watu wa undugu au jamii moja. Katika mada hii utaweza kujifunza muundo wa uandishi wa barua ya kirafiki na jinsi ya kuandika barua ya kirafiki. Utaweza kutofautisha kati ya barua ya kirafiki na ile isiyokuwa ya kirafiki.   BARUA ZA KIRAFIKI   Iwapo ni katika ndugu barua za kirafiki zaweza kuwa kwa watu kama: baba, mama, shangazi, mume, mke, mtoto, na kadhalika. Katika jamii waandikiwao barua za kirafiki ni kama jirani, rafiki, mpenzi, mwalimu, mwanafunzi, daktari, mgonjwa, na kadhalika.   Muundo wa Barua za Kirafiki   Mambo muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa barua za kirafiki:   1. ANWANI kamili ya mwandishi, katika herufi hukaa juu upande wa kulia mwa karatasi.   2. TAREHE, chini ya anwani.   3. MTAJO wa heshima kwa anayeandikiwa, kama vile, mpendwa, mpenzi, na kadhalika, huandikwa kushoto, baada ya tarehe.   4. UTANGULIZI wa baru

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA - USIMULIZI

  USIMULIZI Usimulizi ni jumla ya maelezo yanayotolewa na mtu au watu wengi kuhusu tukio fulani. Katika mada hii utajifunza juu ya taratibu za usimulizi wa matukio kupitia njia kuu mbili za masimulizi, yaani kwa njia ya mdomo au kwa njia ya maandishi. Pia utaweza kujifunza juu ya mbinu mbalimbali za usimulizi.   USIMULIZI WA HADITHI   Usimulizi hufanyika kwa njia kuu mbili yaani kwa njia ya maandishi na kwa njia ya masimulizi ya mdomo. Kila njia hutegemea namna msimuliaji anavyoweza kuwasiliana na msikilizaji. Ikiwa msimuliaji na msikilizaji hawakukaribiana, njia ambayo itatumika ni ile ya maandishi. Kwa mfano kama utahitaji kumweleza mtu aliyembali kuhusu tukio fulani la kusisimua utalazimika kutumia maandishi, yaani utatumia njia ya kumwandikia barua. Lakini kama unamsimulia mtu ambaye yupo karibu nawe, utatumia njia ya mazungumzo ya ana kwa ana. USIMULIZI WA HABARI   Taratibu za Usimulizi wa Matukio: Usimulizi wa matukio dhamira yake ni kumweleza mtu au watu tu

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA - FASIHI KWA UJUMLA

    FASIHI KWA UJUMLA   Fasihi  ni sanaa ya lugha inayoshughulikia masuala yanayomhusu binadamu matatizo yake, ndoto zake, matumaini yake, migogoro yake na jinsi anavyoingiliana na mazingira yake. (Wamitila, 2004). Fasili hii imejaribu kufafanua vizuri kile ambacho fasihi inajihusisha nacho, kimsingi fasihi inajihusisha na wanadamu. Vitu vya msingi tunavyoviona katika fasili hii ni kwamba fasihi ni sanaa, na fasihi inatumia lugha lakini zaidi fasihi inajihusisha na wanadamu. Dhima za Fasihi katika Jamii Dhima za fasihi katika jamii ni pamoja na hizi zifuatazo: 1.   Kuburudisha jamii : Pamoja na mambo mengine fasihi inalenga kuburudisha jamii. Kupitia takribani vipera vyake vyote, fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira, kwa mfano kupitia nyimbo, hadithi, mashairi na kadhalika. 2.   Kuelimisha .  Fasihi hutumika kama nyenzo ya kuelimisha jamii, kupitia fasihi wanajamii wanaweza kuelimishwa juu ya mambo mabalimbali, kama vile

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA - AINA ZA MANENO

AINA ZA MANENO Katika lugha ya Kiswahili kuna angalau aina nane za maneno ambazo wataalamu wengi wa lugha wanakubaliana hivyo. Katika mada hii utaweza kujifunza na kubainisha aina zote nane za maneno na jinsi zinvyotumika katika sentensi. Utaweza pia kujifunza namna ya kutofautisha aina za maneno ambazo zimeleta ubishi miongoni mwa wataalamu wengi hususani katika Viunganishi na Vihusishi.   Aina Saba za Maneno ya Kiswahili                                             Aina za maneno katika lugha ya Kiswahili ni pamoja na hizi zifuatazo:   Aina Nomino (N)                                                                                                       Viwakilishi (W)    Vitenzi (T)                                                                                                                 Vivumishi (V)    Vielezi (E)  Viunganishi (U)   Vihusishi (H) Vihisishi (I)   Ufafanuzi wa Aina za Maneno   1.   NOMINO (N)   Nomino ni maneno yanayotaj

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA - FASIHI SIMULIZI

  FASIHI SIMULIZI   Fasihi simulizi ni moja kati ya tanzu za fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo. Katika mada hii utajifunza na kisha utaweza kubainisha tanzu na vipera vya fasihi simulizi pamoja na ufafanuzi wake. Na pia utaweza kutofautisha kati ya kipera na kipera au kati ya utanzu na utanzu.   Tanzu za Fasihi Simulizi   Fasihi Simulizi ni kazi ya fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo kama vile; hadithi, ngoma na vitendawili.   Tanzu za Fasihi Simulizi ni pamoja na hizi zifuatazo: - Masimulizi/hadithi  - Semi - Ushairi - Mazungumzo - Maigizo  - Ngomezi   Vipera vya Tanzu za Fasihi Simulizi   1.  SIMULIZI/ HADITHI   Masimulizi ni fasihi yenye kusimulia habari fulani. Ni masimulizi ambayo yanatumia lugha ya mjazo au nathari na mtiririko wake huwa mwepesi au sahili. Urefu wa hadithi hutofautiana kutoka kitanzu/kipera kimoja hadi kingine. Kwa jumla zi

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA - MAWASILIANO

MAWASILIANO Katika mada hii unatarajiwa kuelewa fasili ya mawasiliano na jinsi mchakato wa mawasiliano unavyofanyika. Utaelewa dhana ya lugha na vipengele muhimu vinavyokamilisha fasili ya lugha. Utaelewa dhima kuu za lugha, matumizi na umuhimu wake. Vilevile katika mada hii utajifunza juu ya lafudhi na matamshi mbalimbali ya watumiaji wa lugha ya Kiswahili. Lugha kama Chombo cha Mawasiliano Mawasiliano ni mchakato wa kuhawilisha taarifa kwa njia ya ubadilishanaji wa mawazo, hisia, malengo, tabia, matarajio, mitazamo kupitia mazungumzo, ishara na maandishi. Ni ubadilishanaji wa taarifa unaoleta maana baina ya pande mbili au zaidi ambazo zinaweza kuwa viumbe hai au kinyume chake. Sasa hapa sisi tutajikita katika mawasiliano yanayofanywa baina ya viumbe wanaotumia lugha (ambao kimsingi ni binadamu). Maana ya Mawasiliano Lugha ni nyenzo muhimu sana katika mawasiliano ya binadamu. Ulishawahi kujiuliza kwamba mwasiliano yangekuwaje pasipokuwepo lugha? Mwalimu angekua anatumia mt